Matumizi ya Mhusika Kipofu katika Filamu za Kiswahili
Abstract
Makala hii inakusudia kuchunguza matumizi ya mhusika kipofu katika filamu za Mboni Yangu (Wastara, 2002), Family Tears (Kanumba, 2008) na Siyabonga (Gabo, 2017). Sababu ya uchunguzi huu inatokana na madai kwamba, walemavu wasioona wana fursa ya kujiingizia kipato na kukuza uchumi binafsi (Chamba, 2011). Madai mengine ni kwamba, watunzi huutumia ulemavu kama mtindo wa kipekee unaomwezesha kuwasilisha ujumbe kwa hadhira lengwa kupitia filamu. Data za makala hii zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya utazamaji na usikilizaji, Nadharia ya Uamilifu iliasisiwa na Bronislaw Malinowski, Auguste Comte, Emile Durhheim na Herbert Spencer katika karne ya 19 ndiyo iliyoongoza ukusanyaji na uchambuzi wa data za makala hii. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa mhusika kipofu katika flamu anatumiwa na mtunzi kwa lengo la kuitazamisha jamii nafasi ya walemavu katika jamii dhidi ya mtazamo hasi wanaojengewa na jamii.
Fields of Study & Subjects
Cinema History and Criticism
Ethics
Aesthetics
and Art
Language and Culture
Publication details
- Journal / source
- East African Journal of Swahili Studies
- Volume
- 9
- Issue
- 1
- Pages
- 1–9
- Publication date
- 9 January 2026