Dhima za Mbinu za Kisanaa katika Kujenga Dhamira katika Diwani ya Wasakatonge (2003) na Chini ya Mwembe (2017)
Abstract
Makala haya yanatalii dhima za mbinu za kisanaa zinavyojenga dhamira katika ushairi wa Kiswahili. Data za msingi za utafiti huu zimepatikana katika diwani za Wasakatonge (2003) na Chini ya Mwembe (2017). Dhima za mbinu za mbinu za kisanaa katika diwani hizi zimejitokeza kutokana na namna washairi walivyotumia vipengele vya kisanaa katika diwani zao. Katika makala haya, tumetumia mbinu ya usomaji makini kwa kusoma na kuchunguza diwani teule. Aidha, uwasilishaji, uchambuzi na mjadala wa data katika utafiti huu umefanywa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na kuongozwa na nadharia ya Uhalisia. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa, mbinu za kisanaa katika diwani teule zinadhima za kudhihirisha masuala mbalimbali kama vile: amali za jamii, siasa na uongozi, imani ya dini, mila na desturi, malezi ya watoto, elimu pamoja majukumu kijinsia.
Fields of Study & Subjects
Poetry Analysis and Criticism
Caribbean and African Literature and Culture
Postcolonial and Cultural Literary Studies
Publication details
- Journal / source
- East African Journal of Swahili Studies
- Volume
- 9
- Issue
- 1
- Pages
- 10–24
- Publication date
- 12 January 2026