Nafasi ya Utoupole Katika Ukuzaji wa Maudhui Katika Tamthilia ya Pango
Abstract
Utoupole ni suala ambalo limetafitiwa na wanazuoni mbalimbali katika filamu, mikutano ya kisiasa na hata kwenye vibandiko vya magari. Makala hii inakusudia kubainisha mchango wa mikakati ya utoupole katika kuendelza maudhui katika tamthilia ya Pango. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya utoupole ya Culpeper (1996). Utafiti huu ulihusisha sampuli lengwa ambayo ni tamthilia ya Pango. Data ilikusanywa kwa kusoma kwa makini tamthilia ya Pango na kunakili kauli zote zenye utoupole. Kisha data ilichanganuliwa kwa kuzingatia mikakati mitano ya utoupole ambayo ni pamoja na: mikakati hasi ya utoupole, mikakati chanya ya utoupole, mikakati ndani ya rekodi ya utoupole, matumizi ya kejeli na kutowasilisha chochote. Utafiti huu utawasaidia wachanganuzi wa fasihi kwa kuonyesha namna nadharia ya isimu inaweza kutumiwa kuchanganua data ya fasihi na hivyo kuonyesha ukuruba uliopo baina ya fasihi na isimu. Utafiti huu unapendekeza uchunguzi zaidi ufanywe kuhusu majukumu mengine ya utoupole katika tanzu zingine.
Fields of Study & Subjects
Syntax
Semantics
Linguistic Variation
Linguistics and Language Studies
Linguistic research and analysis
Publication details
- Journal / source
- East African Journal of Swahili Studies
- Volume
- 9
- Issue
- 1
- Pages
- 25–33
- Publication date
- 19 January 2026