Dhima ya Deksia katika Kujenga Mshikamano wa Matini Teule

Read full text
Authors: Cheruiyot Evans Kiplimo, Peter Githinji, Leonard Chacha Mwita
Cited by: 0

Abstract

Makala hii inachunguza nafasi ya deksia katika kujenga mshikamano katika hotuba za mijadala ya Bunge la Mwananchi (BLM), Jacaranda. Mshikamano katika Kiswahili umeshughulikiwa kwa kuegemea matawi ya isimu ya semantiki na sintaksia. Makala hii inasisitiza kuwa, mshikamano hauletwi na uzingativu wa semantiki na sintaksia pekee. Mshikamano wa kisarufi kupitia kwa urejeshi unategemea deksia ambacho ni kipengele cha pragmatiki. Isitoshe, tafiti zinazohusu deksia zimeangazia aina zake na takwimu zinazohusu utokeaji wake katika diskosi mbalimbali bila ya kuzingatia uamilifu wake katika matini. Hivyo, makala hii imechunguza nafasi ya deksia katika kukuza mshikamano kwa kuongozwa na nadharia ya Sarufi Amilifu Mfumo (S.A.M) ya Halliday (1985) kwa mtazamo wa maana matinishi. Maana matinishi inaelekeza namna ya kupanga matini katika kifungu na mtagusano kati yao. Data ya makala hii imekusanywa kutoka kwa mtandao wa kijamii wa Youtube. Hotuba teule zilikuwa katika mfumo wa video na zilibadilishwa katika umbo la kimatini kwa mbinu ya kusikiliza, kutazama na kunakili. Data ilihifadhiwa katika programu ya Microsoft Word kisha ikagawanywa katika makundi madogo ya vifungu, sentensi na vishazi na kuchanganuliwa kwa kuongozwa na kishazi, kipashio muhimu cha Sarufi Amilifu mfumo. Makala hii imebaini kuwa deksia inakuza mshikamano kwa njia mbalimbali ikiwemo: kushiriki na anafora, kufuatilia washiriki na majukumu yao katika diskosi, kuondoa utata katika matini na kuingiliana na mshikamano wa kisarufi. Makala hii inatoa mchango katika tawi la isimu matini, semantiki na pragmatiki

Fields of Study & Subjects

Syntax Semantics Linguistic Variation Linguistics and Discourse Analysis Discourse Analysis in Language Studies

Publication details

Journal / source
East African Journal of Swahili Studies
Volume
9
Issue
1
Pages
88–105
Publication date
3 February 2026