Nahau na Ujenzi wa Mshikamano katika Matini Teule

Read full text
Authors: Cheruiyot Evans Kiplimo, Peter Githinji, Leonard Chacha Mwita
Cited by: 0

Abstract

Makala hii imechunguza namna nahau inakuza mshikamano katika hotuba za mijadala ya Bunge la Mwananchi (BLM), Jacaranda. Ili matini yawe na mshikamano, maneno yenye mahusiano ya moja kwa moja na yenye kuhusiana na muktadha hutumika. Hata hivyo, sio kila mara hili linatokea haswa pale ambapo kuna matumizi ya nahau. Nahau huwa na ubuye wa kisemantiki; yaani, maana ya nahau huwa haihusiani na maana za maneno yaliyotumiwa. Hivyo, makala hii imechunguza nahau za Kiswahili kwa lengo la kuelewa jinsi zinavyoshiriki katika kujenga mshikamano na kupanga ujumbe au matini kwa jumla kwa kuongozwa na nadharia ya Sarufi Amilifu Mfumo (SAM) ya Halliday (1985) katika mtazamo wa maana matinishi. Maana matinishi ni uamilifu unaohusika na ujenzi wa matini na kupanga maana dhanishi na maana kijamii kama diskosi. Data ya makala hii imekusanywa kutoka kwa mtandao wa kijamii wa Youtube. Hotuba 12 za mijadala ya Bunge la Mwananchi zilisampuliwa kimakusudi kwa kuwa zinasheheni nahau. Kusikiliza, kutazama na kunakili ndizo mbinu kuu zilizotumika kubadili video hadi umbo la kimatini. Nahau ilichanganuliwa katika muktadha wa matinishirikishi. Imebainika kuwa nahau inajenga mshikamano wa kileksia kupitia kwa maneno tangamano na urudiaji. Isitoshe, nahau inaandaa mazingira ya utumiaji wa vipengele vya kisarufi vya mshikamano kama vile urejeleaji na uunganishaji katika matini-shirikishi. Aidha, baadhi ya viambajengo vya nahau vimebadilishwa ili viendane na muktadha wa matini-shirikishi. Makala hii inatoa mchango katika tawi la isimu matini, sintaksia, semantiki na pragmatiki

Fields of Study & Subjects

Linguistics and Discourse Analysis Language Discourse Communication Strategies Linguistic research and analysis

Publication details

Journal / source
East African Journal of Swahili Studies
Volume
9
Issue
1
Pages
106–121
Publication date
3 February 2026