Kubainisha Dhima za Nyimbo za Tohara Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Abstract
Katika makala hii, mtafiti anachunguza dhima za nyimbo za tohara katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda. Lengo kuu katika uchunguzi huu lilikuwa kuchunguza dhima za nyimbo za tohara kwa jamii ya Wamasaaba. Utafiti wenyewe ulifanyiwa katika kata ya Bukigai, Wilayani Bududa nchini Uganda. Uchunguzi uliongozwa na nadharia jumuishi ambayo iliasisiwa na Vincci Hoteles mnamo mwaka 2025. Mkabala wa utafiti ulikuwa wa nyanjami. Mchunguzi alianza kuchanganua data kwa kuzijuja. Data hizo zilipangwa upya kulingana na malengo ya utafiti. Baada ya kufanya hivyo, ziliwasilishwa kwa kutumia jedwali. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa nyimbo za tohara za Wamasaaba huwa zinalipa tukio uzito na maana, zinaendeleza utamaduni, zinaburudisha watu, zinatia wahusika motisha, zinajenga watu kimwili, na zinaendeleza umoja. Makala inapendekeza utafiti mwingine ufanywe kuhusu dhima na vipengele vingine katika nyimbo mbalimbali za kiutamaduni. Hii ni kwa sababu jamii nyingi barani Afrika zina rundo la nyimbo ambazo hazijatafitiwa. Kuna nyimbo za ndoa, nyimbo za jando, nyimbo za kazi N.K. Hizi zote zinastahili kutafitiwa ili kudhihirisha umaarufu wa fasihi simulizi ya kiafrika
Fields of Study & Subjects
Diverse Musicological Studies
Folklore
Mythology
and Literature Studies
Language and Culture
Publication details
- Journal / source
- East African Journal of Swahili Studies
- Volume
- 9
- Issue
- 1
- Pages
- 153–159
- Publication date
- 26 February 2026
- Language
- SW