Tafsiri na Ukalimani katika Diplomasia na Mahusiano ya Kimataifa
Abstract
Katika Makala hii, mtafiti anaeleza dhima za huduma za tafsiri na ukalimani katika diplomasia na mahusiano ya kimataifa. Kwa kurejelea dhima hizo, mtafiti anafafanua namna huduma za tafsiri na ukalimani zinaweza kuwa na manufaa katika shughuli za kimataifa. Hii ni kwa sababu katika ulimwengu wa sasa, mataifa huwa yakishirikiana katika mambo tofautitofauti na kuna mahitaji ya kuwasiliana vilivyo. Ili kuwafanya wanadiplomasia waelewane katika mikutano yao, wanapaswa kutumia tafsiri na ukalimani. Makala hii iliongozwa na nadharia ya kimawasiliano na tafsiri. Kulingana na nadharia hii, katika tafsiri, ni maana inayohamishwa wala si lugha. Hii ni kwa sababu lugha huwa kama chombo kinachosafirisha ujumbe na hata inaweza kuwa kizuizi katika ufahamu wa wasomaji. Hii ndiyo sababu kwenye tafsiri, wafasiri hawawezi kufasiri neno kwa neno. Suala la utafiti katika makala hii ni kuwa tafsiri na ukalimani ni muhimu sana katika masuala ya kibiashara na diplomasia lakini mara nyingi dhima za huduma hizi mbili hazionekani na hazithaminiwi. Lengo kuu katika makala hii, ni kueleza dhima za tafsiri na ukalimani katika diplomasia na mahusiano ya kimataifa. Mkabala wa utafiti huu ulikuwa wa kimaelezo. Kwa kutumia mkabala huu, mtafiti alipekua majarida mbalimbali na kusoma machapisho ya watafiti tofauti. Taarifa zilizokusanywa zilichanganuliwa na kuwasilishwa kimaelezo. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa tafsiri na ukalimani hufanikisha mawasiliano, mapatano, kusaini mikataba, kwendeleza biashara, huwa kama daraja linalounganisha wanadiplomasia n.k.
Fields of Study & Subjects
Translation Studies and Practices
Language
Communication
and Linguistic Studies
Interpreting and Communication in Healthcare
Publication details
- Journal / source
- East African Journal of Swahili Studies
- Volume
- 9
- Issue
- 1
- Pages
- 160–173
- Publication date
- 26 February 2026
- Language
- SW